“Ikiwa Wazanzibari wataukataa Muungano, bila mashinikizo kutoka mataifa ya nje, siwezi kuwapiga mabomu kuwalazimisha.”

Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kueleza nia yake ya wazi kuwa ikiwa Wazanzibari wanaona hawautaki Muungano hawezi kuwazuia.

 

 

Machel: urafiki si hisani

“Umoja katika katika jamii ya kimataifa si hisani; Ni tendo la umoja kati ya wabia wanaopambana katika majukwaa tofauti kutimiza lengo moja. Kubwa kuliko yote ni kusaidia maendeleo ya binadamu kwa kiwagno cha juu.”

Haya ni maneno yalisemwa na aliyekuwa Rais wa Msumbiji wa Samola Machel kusisitiza umuhimu wa mataifa kuwa wamoja.


Adams: Kalamu si mchezo

“Bila shaka kalamu ni silaha muhimu kwa binadamu kuweka nia yake na kuamsha matarajio.”

Haya ni maneno ya Rais wa Marekani John Adams aliyetawala kati ya 1797–1801, aliyetaka viongozi wenzake wasipuuze wanahabari.


Mkapa: Mtaji wa maskini

“Tuache uvivu wa kufikiri. Yatupasa sasa kila mtu kufanya kazi, kwani bila kufanya hivyo watu wa kuwaomba hawapo tena. Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.”

Haya ni maneno ya Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa wakati akiwasihi Watanzania kufanya kazi bila kuchoka kipindi akiwa Rais wa Tanzania