“Vyombo vya umma vitumiwe kuhudumia wananchi. Wote wanaoviharibu ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi, lazima wajisahihishe; la sivyo wanyang’anywe madaraka.”

Ni maneno ya mwasisi na Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, alipowaasa viongozi kutumia vizuri madaraka yao kwa kuhakikisha vyombo vya umma vinahudumia wananchi kwa uzito unaostahili.

Nyalali: Hakimu na haki

“Ni afadhali kuwa na hakimu asiyejua sheria anayetenda haki, kuliko kuwa na hakimu anayejua sheria asiyetenda haki.”

Kauli hii ni ya Jaji Mkuu, Francis Nyalali, alipohudumia umma akisisitiza dhana ya kutoa hukumu za haki mahakamani.

 

Thiong’o: Ukoloni wa fikra

“Ukoloni wa kifikra walionao viongozi wetu, unaweza kuleta machafuko kwa siku za usoni hasa kwa kuwa rasilimali zimekuwa zikitolewa kwa wageni huku wazawa wakibaki kuwa vijakazi.”

Haya ni maneno ya mtunzi gwiji wa vitabu barani Afrika, Profesa Ngugi wa Thiong’o, katika moja ya vitabu vyake.

 

Kikwete: Uhuru wa mawazo

“Ninasemwa sana kwa sababu nimetoa uhuru mkubwa sana kwa vyombo vya habari na wanasiasa…”

Maneno haya ni ya Rais Jakaya Kikwete, alipohutubia Watanzania, akielezea uvumilivu wake katika masuala ya siasa na utawala.