“Kipimo kingine cha CCM ni kwamba hatujaweza kujitegemea kwa fedha. CCM inapata ruzuku kubwa kutoka serikalini, na maana yake ni kwamba inachukua kodi za wananchi wote, wanachama na wasiokuwa wanachama.”
Maneno haya ni ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere, wakati akihutubia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Taifa, jijini Dar es Salaam, Agosti 16, 1990.
Rohn: Lengo la uongozi
“Lengo zuri la uongozi ni kuwasaidia wale ambao wanafanya vibaya wafanye vizuri na kuwasaidia wale ambao wanafanya vizuri kufanya vizuri zaidi.”
Haya ni maneno ya mjasiriamali maarufu wa nchini Marekani, Jim Rohn, wakati akielezea majukumu ya viongozi katika jamii.
Mwai Kibaki: Fursa ya uongozi
“Uongozi ni fursa ya kuboresha maisha ya wengine. Siyo nafasi ya kukidhi tamaa binafsi.”
Hii ni kauli ya Rais Mwai Kibaki wa Kenya, wakati akiwakumbusha viongozi kutambua wajibu wao wa kuboresha maisha ya wananchi na kuepuka kutanguliza maslahi yao binafsi.
Kagame: Nguzo ya maendeleo
“Katika Afrika ya leo, tunatambua kwamba biashara na uwekezaji, na si misaada, ni nguzo ya maendeleo.”
Rais Paul Kagame wa Rwanda, aliyasema haya wakati akielezea umuhimu wa biashara na uwekezaji katika nchi zinazoendelea.