“Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni; tatizo ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo… Panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni.”
Haya ni maneno ya Baba wa Taifa letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakati akifafanua jinsi ilivyo vigumu kwa panya kuepuka kukamatwa na paka.
Angelou: Ujasiri na fadhila
“Ujasiri ni muhimu zaidi kuliko fadhila zote, kwa sababu bila ujasiri daima, huwezi kufanya fadhila nyingine yoyote. Unaweza kufanya fadhila yoyote kimakosa, lakini bila ujasiri daima hakuna chochote.”
Haya yalisemwa na mwandishi wa vitabu na mshairi maarufu mwanamke wa nchini Marekani, Maya Angelou, wakati akihimiza watu kujenga dhana ya ujasiri katika utendaji.
Gates: Sherehe na mafanikio
“Ni vizuri kusherehekea mafanikio, lakini ni muhimu zaidi kujua masomo ya kushindwa.”
Kauli hii ilitolewa na mfanyabiashara tajiri na mtoaji misaada maarufu wa nchini Marekani, Bill Gates, wakati akisisitiza umuhimu wa kusherehekea mafanikio na umakini juu ya masomo magumu.
Nkrumah: Mapinduzi na watu
“Mapinduzi yanaletwa na watu wanaofikiri kama watu wa vitendo na kutenda kama watu wa kufikiri.”
Kwame Nkrumah, Rais wa zamani wa Ghana, aliyasema haya kubainisha aina ya watu wanaostahili kuleta mabadiliko yenye manufaa katika jamii.