Julius Nyerere: Tujifunze kusikiliza hoja za wengine

“Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zilizotolewa na wenzetu, na kuzijibu kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama aliyezitoa ni rafiki au si rafiki.”


Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.

Indira Gandhi: Jikite katika kundi la kufanya kazi

“Kuna wakati babu yangu aliniambia kwamba kuna aina mbili za watu; wale ambao hufanya kazi na wale ambao hupata sifa. Aliniambia nijaribu kuwa katika kundi la kwanza; ambako kuna ushindani mdogo.”


Haya yalisemwa na Indira Priyadarshini Gandhi, Waziri Mkuu wa tatu wa India. Alipata kutunukiwa Tuzo ya Amani ya Lenin.

 

Robert Mugabe: Tunawakaribisha Wazungu wanaozingatia usawa

“Wazungu ambao wanaoonekana kuwa hapa nchini [Zimbabwe] na wanajishughuli na kilimo wanakaribishwa kufanya hivyo, lakini lazima wafanye hivyo katika misingi ya usawa.”


Hii ni kauli ya Rais wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe. Analiongoza taifa hilo tangu mwaka 1980.

 

Melinda Gates: Mafanikio yana mkono wa mtu

“Kama unafanikiwa, hiyo ni kwa sababu mahali fulani, wakati fulani, mtu fulani alikupa maisha au wazo ambalo lilikuanzishia mwelekeo sahihi.”


Kauli hii ni ya mfanyabiashara Melinda Gates, ambaye ni mke wa mfanyabiashara bilionea maarufu wa nchini Marekani, William Henry “Bill” Gates.