Nyerere: Wanadamu huongozwa na sheria

“Nchi zote duniani huongozwa na wanadamu na si malaika. Wanadamu hawa huongozwa na Sheria na si kwa akili zao wenyewe.”

 

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyasema haya wakati akihimiza Watanzania kulinda Katiba na sheria za nchi.

 

Papa Benedict XVI: Tuheshimu wanaoteseka

“Lazima tuwe na heshima kubwa kwa hawa watu ambao pia wanateseka na wanaotaka kupata njia yao wenyewe ya maisha sahihi.”

 

Haya ni maneno ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani aliyejiuzulu mwezi uliopita, Papa Benedict XVI.

 

Sharapova: Napenda kuwa tofauti

“Napenda kuwa tofauti. Kama kila mtu anavaa nyeusi, mimi napenda niwe nimevaa nyekundu.”

 

Hii ni kauli ya mchezaji maarufu wa tenisi duniani, Maria Sharapova wa nchini Urusi. Machi 4, mwaka huu, aliibuka mshindi wa tatu katika mashindano ya kimataifa.

 

Kagame: Tukazanie biashara, uwekezaji

“Katika Afrika ya leo, tunatambua kwamba biashara na uwekezaji, sio misaada, ni nguzo za maendeleo.”

 

Maneno haya ni ya Rais Paul Kagame wa Rwanda, wakati akihamasisha ukuzaji uchumi kupitia biashara na uwekezaji.