Nyerere – Siasa za ndani

“…Mtu yeyote anayetuvurugia umoja wetu si mwenzetu. Hata angevaa ngozi ya kondoo huyu ni mbwa mwitu hatufai hata kidogo.”

Nukuu hii ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilichukuliwa katika ukurasa wa 111 katika kitabu cha Nukuu za Kiswahili za Mwalimu Nyerere, aliyezaliwa mwaka 1922. Alifariki dunia Oktoba 14, 1999.

***

Dk. Magufuli – Hazina

Watanzania tuna mali nyingi lakini tunazichezea mpaka shetani anatucheka huko aliko.”

Nukuu hii ilitolewa na Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, wakati akipokea ripoti ya uchunguzi ya madini.

***

Kagame – Uwekezaji, biashara

Katika Afrika ya leo, tunatambua kwamba biashara na uwekezaji siyo msaada, ni nguzo za maendeleo.”

Nukuu hii ilitolewa na Rais wa Rwanda, Paulo Kagame, wakati akihamasisha ukuzaji wa uchumi kupitia biashara na uwekezaji.

***

Karl Marx – Mtaji

Mtaji ni nguvukazi iliyokufa, ambayo ni kama mnyonya damu anayeishi tu kwa kunyonya nguvukazi iliyo hai, na anaishi zaidi kadiri anavyonyonya nguvukazi nyingi.”

Nukuu hii ilitolewa na  mwanafalsafa wa Kijerumani, Karl Marx, aliyeandika machapisho mengi duniani akipinga dhana ya unyonyaji na kuamini katika usoshalisti.