đź“ŚNIRC, Monduli

SERIKALI ya Awamu ya Sita ,kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), imesaini Mkataba Wa kukarabati skimu zilizopo katika bonde la Mto wa Mbu Wilayani Monduli, kwa gharama ya shilingi bilioni 17

Mradi huo unajumuisha ukarabati wa mifereji yenye urefu wa jumla ya Mita 37,484.71, sawa na urefu wa zaidi ya Kilomita 37.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, amewataka wananchi wa eneo la mradi kuwa macho dhidi ya watu wasiowaaminifu katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo

“Mradi huu unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo na mifugo katika bonde la Mto Wammbu, na kuondoa changamoto za muda mrefu zilizokuwepo katika jamii hizo,”amesema.

Nao Wananchi wanaotoka katika kata ya Mto wa Mbu, ambapo skimu hiyo inapatikana, wamepata tumaini jipya la kuimarisha kilimo na kuondokana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Wakazi hao wameishukuru serikali kwa hatua iliyofikiwa na wameahidi kushirikiana na serikali katika kuulinda mradi na kutoa taarifa, ikiwa watabaini viashiria vyovyote vya kuhujumu mradi huo.

Baadhi ya wananchi jamii ya Wafugaji wanaotoka karibu na eneo la mradi akiwemo Dorah Mbwambo amepongeza mradi huo wakisema utasaidia kukomesha migogoro kuhusu maeneo ya kunyweshea mifugo na maeneo ya kilimo na kwamba ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika eneo hilo, itakuwa msaada mkubwa katika kudhibiti mafuriko ambayo yamekuwa tishio kwa wakazi hao, kwa miaka mingi.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga, amesema mradi huo ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi hao na halamshauri itahakikisha inashirikiana na Tume kuusimamia.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo, Fredy Lowasa, wamehimiza uadilifu katika usimamizi wa mradi huo, ili uweze kuleta tija iliyokusudiwa

Bonde la Mto wa Mbu lina ukubwa wa Hekta 4,000 sawa na ekari 10,000 na linatarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 20,000, huku likihudumia Skimu za Umwagiliaji zaidi ya 12.Skimu hizo ni Majengo juu,Kabambe,.miwaleni, Mkombozi(Block Farm),Migombani juu, Migombani kati, Migombani chini,mahande ,migungani , kirurumo , Jangwani na Mungere.Mazao yanayolimwa katika bonde la Mto Mbu ni Migomba, Mpunga, Mboga mboga, viazi, maharage na miwa. ‎