Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeshiriki ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutembelea mradi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika shamba la mbegu la Wakala wa Mbegu (ASA) lililopo Ngaramtoni, eneo lililowekewa miundombinu ya Umwagiliaji Hekta 160 kati ya 200 sawa na asilimia 82 ya utekelezaji, na shamba la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika kituo cha TARI kilichopo Seliani mkoani Arusha.

Katika utekelezaji mradi huo Tume imeshiriki Kama mshauri mwelekezi katika usimamizi wa mradi.

Aidha kamati hiyo imeipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuwa wabunifu na mipango madhubuti ya kuhakikisha inakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwekeza katika sekta ya Umwagiliaji na kuongeza Uzalishaji.