Na Isri Mohamed
Katika hali ya kushangaza timu ya taifa ya Nigeria imeamua kurejea nchini kwao bila kucheza mchezo wao wa kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Libya, baada ya kufanyiwa vitendo ambavyo wamevitafsiri ni hujuma kutoka kwa wenyeji wao Libya.
Ndege maalumu iliyobeba wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na watu wengine walioambatana na timu ya taifa ya Nigeria ilizuiwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Benina mji ambao mechi ilipangwa kuchezwa badala yake ikaelekezwa itue kwenye mji wa Al Abaq ambao una umbali wa (KM 230) kutoka Benina.
Sababu ya kuambiwa wakatue mji wa Al Abaq ni kujaa kwa uwanja wa ndege wa mji wa Benghazi Kila walipoulizia kurusha ndege kutoka Al Abaq kwenda Benina waliambiwa bado uwanja wa ndege hauna nafasi hivyo wanapaswa kusubiri.
Inaelezwa watu wote waliokuwa kwenye ndege wakiwemo wachezaji walikwama uwanja wa ndege wa Al Abaq kwa zaidi ya saa 13 bila kula chochote, Vilevile wachezaji wa Nigeria wanadai kwamba walikuwa wanasachiwa na maofisa wa Libya.
Kufuatia tukio hilo Nahodha wa Nigeria, Troost-Ekong ametangaza rasmi kwamba hawatacheza mchezo huo na kusema.
“Kwa zaidi ya masaa 12 tumetelekezwa katika uwanja wa ndege huko baada ya ndege yetu kubadilishiwa uelekeo. Serikali ya Libya itabatilisha eneo letu lililoidhinishwa kutua huko Benghazi bila sababu.”
Katika hatua nyingine nahodha wa timu ya taifa ya Libya Al Badri amesema kilichowatokea Nigeria kiliwatokea wao pia walipofika Nigeria kabla ya kusaidiwa na magari mawili kutoka kwa ubalozi wa Libya baada ya saa nyingi kuzunguka uwanja wa ndegeā¦