Rais wa Venezuela Nicolás Maduro, ameshinda uchanguzi kwa awamu ya sita kwenye uchaguzi uliokubwa na ususiaji kutoka chama kikuu cha upizani kwa madai ya udanganyifu wa kura.
Kutokana na upungufu wa chakula unaosababishwa na changamoto za kiuchumi , asilimia 46, ya wapinga kura ndio waliojitokeza na kupiga kura.
Mpizani mkuu Henri Falcon , alipinga matokeo hayo punde tu baada ya vituo vya upigaji kura kufungwa.
”Hatutambui kama uchanguzi huu ulikuwa halali …lazima tuwe na uchaguzi mpya nchini Venezuela ,”alisema.
Kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura zilizohesabiwa , Bw Maduro, 55, alipata asilimia 67.7 kwa kura milioni 5.8-Chifu wa Baraza la Taifa la Uchaguzi Tibisay Lucena alitangaza.
Bw Falcón alishinda kwa asilimia 21.2 – kwa kura milioni 1.8 alisema.
”Walinidharau mimi,”Bw Maduro aliwahutubia wafuasi wake nje ya kasri ya rais huko Caracas, pale fataki zilipozimwa na katarasi zenye rangi tofauti kupeperushwa angani.
Bw Falcón anadai kwamba kura hizo ziliibiwa ili kumnufaisha Bw Maduro, kwa kutumia vibaya kadi za taifa zinazotumika kupata chakula.
Maafisa wa serikali walisema kwamba uchaguzi huo ulikuwa wa ”huru na haki” lakini wapinzani wengi walisusia upigaji kura.
Afisi wa utawala wa rais wa Marekani Donald Trump imesema haitatambua matokeo hayo. Kwenye mtandao wa Twitter uliochaishwa kabla upigaji kura kuanza nchini humo , Ujumbe wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa wameutaja uchaguzi huo ”dharau kwa demokrasia.”
Uchaguzi huo ulistahili kufanyika mwezi Disemba 2018, lakini Baraza la Majimbo la Taifa,liliobuniwa kwa maalum na wafuasi wa Bw Maduro, ulisongeza mbele uchaguzi huo.
Muungano wa upizani wa Democratic Unity ulisema uchaguzi ulifanyika ili kutumia nafasi hiyo ya mgawanyiko uliokuwa katika muungano huo. Wagombea wawili wakuu pia walizuiliwa kugombea huku wengine wametoroka nchini humo.
Kuna wagombea wachache lakini Bw Falcón, gavana aliyeongoza wakati wa hayati rais Hugo Chávez, alionekana kama mpizani bora kwa rais Maduro. Falcón, alikuwa chama kimoja cha kisosholisti na rais Maduro, lakini alikiaga chama hicho na kujiunga na upizani mwaka 2010.
Bw Falcón, aliyegombea licha ya ususiaji wa uchaguzi huo , amesema anaamini kwamba raia wengi wa Venezuela wanataka kumuondoa Bw Maduro madarakani.
Wapizani wenzake, hata hivyo, wamekasirishwa na kutosikizana na wenzake – huku wengine wakimtaja kama msaliti.