Mradi wa kuongeza uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili kufikia uhifadhi wa mahndi kutoka tani 251 mpaka tani laki 501 miradi mitatu ya maghala ya kisasa ya kuhifadhia mazao imekamilika na imekabidhiwa kwa NFRA tayari kwa ajili ya kupokea shehena zaidi ya mahindi katika msimu huu wa mavuno.
Ujenzi huo wa maghala umekamilika katika miradi ya Babati mkoani Manyara, Mradi wa Kanondo Sumbawanga mkoani Rukwa na mradi wa Mpanda mkoani Katavi na tayari mkandarasa ameshakabidhi maghala hayo hayo ya Kiasasa kwa ajili ya kuhifadhi mahindi.
Kauli hiyo imetolewa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bw. Milton Lupa wakati akizungumza katika Maonesho ya Kilimo-Nane Nane Kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.
Lupa amesema katika miradi mingine mitano iliyobaki inanatarajiwa kwamba baada ya majadiliano na serikali Mkandarasi ifikapo juni 2023 inaweza kuwa tayari imekamilika ukiacha miradi mitano ambayo ilisimama kwa muda.
Katika miradi hiyo mitano mkandarasi aliyekuwa akitekeleza miradi ile aliondoka eneo la mradi akawa anadai asilimia 73 ya nyongeza ya fedha lakini serikali iliona siyo jambo zuri hivyo iliunda kamati ya majadiliano na mkandarasi na majadiliano yamefanyika wamefikia mahali pazuri ni imani yetu sasa serikali itatoa mwelekeo wa kuendeleza miradi hiyo hivi karibuni kwa sababu serikali imeshamalizana naye.
Amesema Miradi iliyokumbwa na changamoto hiyo ni Mradi wa Songwe mkoani Songwe, Mradi Dodoma mkoani Dodoma, Mradi wa Songea mkoani Ruvuma, mradi wa Shinyanga mkoani Shinyanga na mradi wa Makambako mkoani Iringa ukamilishaji wake utaanza wakati wowote kutokana na serikali kumalizana na mkandarasi
“Katika maonesho haya ya wakulima Nanenane (NFRA) tumeleta elimu kwa wakulima kuhusu njia nzuri za kisasa na za kienyeji namna ya kutambua kama mahindi yamekauka ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kuhifadhi chakula kwa njia za kisasa na za kienyeji ili kuhifadhi mahindi katika njia inayosaidia kupunguza upotevu wa mahindi,” amesema Bw. Milton Lupa.
Aidha ametanabaisha kwamba (NFRA) inawataarifu wakulima kwamba imeleta njia ya Kuhifadhi mahindi katika Maghala ya kisasa na vihenge vya kisasa ili kuongeza uwezo zaidi wa hifadhi chakula nchini.
Ameongeza kwamba mwaka huu wa mavuno Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) itawapa wakulima bei nzuri ya mahindi ili wakulima waweze kupata fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo ili kuendeleza shughuli zao za kilimo kwa tija.
Hivyo amewakaribisha wakulima kuchangamkia fursa hiyo kwa kupeleka mazao yao na kuuza kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) katika maeneo mbalimbali ambayo vituo vya kununulia mahindi vipo.