Na Richard Mrusha, JamhuriMedia, Dodoma

WAKALA wa Uhifadhi wa Chakula Nchini (NFRA) ,umeanza kutumia mfumo wa kidijitali katika kupima mazao ya Nafaka ili kuleta tija kwa wakulima.

AFISA Mtendaji Mkuu wa NFRA Dkt.Andrew Komba ameyasema hayo katika maonesho ya wakulima na wafugaji Wavuvi viwanja vya Nane nane Nzuguni jijini Dodoma yaliyoanza Agosti Mosi na kufikia kilele chake Agosti 8 mwaka huu.

Amesema mizani hiyo inaonesha namna ambavyo mkulima atapata faida na uhakika wa mazao anayouza NFRA.

“Wakulima wameipokea mizani hii vizuri wakiamini kwamba inawawezesha kupata kiwango sahihi wanachotuuzia na sisi kwetu inatupa kumbukumbu’ sahihi kwa sababu inaingiza taarifa katika mfumo ambao unatumika katika suala zima la kuhifadhi .”amesema Dkt.Komba

Aidha amesema ,Wakala huo una jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa na usalama wa chakula .

Kwa mujibu wa Dkt.Komba,ili kulitekeleza jukumu hilo NFRA wamekuwa wakinunua na kukusanya chakula na kuhifadhi vizuri kwa utaratibu wa kuhakikisha afya na usalama wa mlaji.

“Kwa ili kuhakikisha chakula kinakuwa salama wakati wote ,tunatumia maghala na vihenge katika kuhifadhi chakula,lakini pia tunawafundisha wakulima kuhifadhi chakula wanacholima katika hali ya usalama badala ya kuhifadhi kizamani.”amesema Dkt.Komba

Amesema chakula wanachohifadhi kinalenga kuisaidia jamii pale panapotokea uhaba wa chakula na kuwafanya wawe na uhakika wa chakula.

Please follow and like us:
Pin Share