Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaani uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita na Uhalifu (ICC) wa kutoa waranti ya kukamatwa kwake akisema ni “chuki” dhidi yake na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.

Alisema ICC inawashtumu kwa kutumia ”uongo” kwamba “tunawalenga raia kimakusudi wakati tunafanya kila tuwezalo kuepusha mauaji ya raia”.

ICC pia ilitoa waranti ya kukamatwa kwa kamanda wa Hamas Mohammed Deif ambaye Israel inasema aliuawa huko Gaza mwezi Julai.

Majaji wa ICC walisema kulikuwa na “sababu za kuridhisha” kuamini kuwa watatu hao “wana kesi ya kujibu” kwa uhalifu wa vita kati ya Israel na Hamas.

Rais wa Marekani Joe Biden aliitaja hatua ya ICC dhidi ya maafisa wa Israel kuwa “ya kuchukiza”.