Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anatarajiwa kutoa ushahidi mahakamani leo wa tuhuma za rushwa.
Waendesha mashtaka wamemshutumu kwa kutoa makubaliano ya kisheria kwa wamiliki wa vyombo vya habari ili kupata habari chanya, na kukubali zawadi na faida za gharama kubwa ili kuendeleza maslahi binafsi ya mtayarishaji wa Hollywood.
Atakuwa kiongozi wa kwanza wa Israel kutoa ushahidi kama mshtakiwa katika kesi ya jinai.
Netanyahu amejaribu mara kwa mara kuchelewesha mchakato huo kutokana na vita vya Gaza na wasiwasi wa kiusalama, lakini wiki iliyopita majaji waliamuru kesi hiyo iendelee.
Mapema , majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu walitoa waranti ya kukamatwa kwa Bw. Netanyahu. Alishtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita.