Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amefanyiwa upasuaji wa tezi dume .

Upasuaji huo umekuja baada ya kugundulika alipata maambukizi kwenye njia ya mkojo.

Kwa mujibu wa madaktari wanaoendelea kumtibu wamesema Waziri Mkuu Netanyahu anaendelea vizuri na matibabu. S

Hatahivyo kufuatia ugonjwa wa Netanyahu, Mshirika mkubwa wa Netanyahu ambaye ni Waziri wa Sheria Yariv Levin amepandishwa cheo kwa muda kushika nafasi ya waziri mkuu Netanyahu.

Hivi karibuni, Benjamin Netanyahu anakabiliwa na matatizo ya afya lakini katika taswira ya umma amejitahidi kuonekana kiongozi mwenye afya.