Baraza la Mitihani NECTA limesitisha utaratibu wa kutangaza shule 10 bora na mwanafunzi bora wa matokeo ya kidato cha nne kwakuwa utaratibu huo hauna tija.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (CSEE) na maarifa (QT) uliofanyika Novemba/Desemba 2022.

”Tulizoea kusikia lugha za Top 10 sijui wasichana wawagaragaza wanaume, tuondokane na mazoea, ukigundua jambo unalolifanya halina tija hauna haja ya kuendelea nalo.

“Kutangaza shule ya kwanza huenda tulikuwa tunakufanyia Marketing kwa kuitaja tu hiyo shule, shule zipo nyingi zaidi ya 18,000, sasa unapotaja moja sidhani kama ina tija” amesema.

Amesema utaratibu huo ulikuwa ukiwanufaisha watu ambao wamefanya mtihani sawa lakini mazingira tofauti.

“Unamtaja mtu kwamba ameongoza katika kundi ambalo pamoja na kwamba wamefanya mtihani huo huo lakini hawakusoma katika mazingira yanayofanana, alafu sasa unampa sifa mtu mmoja” amesema.

https://matokeo.necta.go.tz/csee2022/index.htm
Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Amasi