Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya ndege ya mizigo kuanguka karibu na uwanja wa ndege wa Vilnius nchini Lithuania

Ndege hiyo, inayoendeshwa kwa DHL na Shirika la Ndege la Uhispania la Swiftair, ilianguka karibu na nyumba wakati ilikuwa inakaribia kutua, mamlaka za eneo zilisema.

Watu wote 12 wameokolewa salama kutoka kwenye maeneo karibu na eneo la ajali, polisi walisema.

Huduma za uokoaji zilisema wale wote waliokuwa kwenye ndege kutoka Leipzig, Ujerumani, wamepatikana.

Ndege hiyo iliondoka kwenye kituo cha DHL kwenye Uwanja wa Ndege wa Leipzig baada ya saa 3:00 saa za ndani (02:00 GMT) na kuanguka karibu saa moja na nusu baadaye, kulingana na data kutoka kwa tovuti ya ufuatiliaji wa ndege ya Flightradar24.

Zima moto walionekana wakikabiliana na moshi kutoka kwenye jengo lililo kilomita 1.3 (maili 0.8) kaskazini mwa barabara ya kurukia ndege, shirika la habari la Reuters liliripoti.

Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana na mamlaka ya Lithuania imeanza uchunguzi.

Mkuu wa kitengo cha kuzima moto na huduma za dharura nchini Lithuania, Renatas Pozela, alisema ndege hiyo ilipaswa kutua katika uwanja wa ndege wa Vilnius na “ilianguka kilomita chache kutoka eneo hilo”.