Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

Katibu Mkuu CCM Taifa ambaye pia ni mgombea mwenza kupitia chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ambao unafanyika kesho mkoani Ruvuma.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Ruvuma leo Aprili 3, 2025 kwenye ukumbi wa mkutano wa hoteli ya Aunt Club ulipo Songea ,Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Parokia Takatifu Manispaa ya Songea kuanzia April 3 hadi 5 ,2025 ambao utaambatana na uchaguzi mkuu wa viongozi wa TEF.

Amezitaja nafasi zinazowaniwa kuwa nafasi ya mwenyekiti ambapo hadi sasa ni mgombea mmoja amerudisha fomu,ambaye ni Deodatus Balile, nafasi ya makamu Mwenyekiti ambayo Bakari Machumu anatetea nafasi yake na ni mgombea pekee aliyerudisha fomu.

Nafasi nyingine ni ya wajumbe kamati tendaji ambapo wajumbe wanahitajika saba lakini waliochukua fomu ni 13 na waliorudisha ni 12 ambapo jumla ya wajumbe 189 wanatarajia kuhudhuria.

Amesema,mkutano huo unatarajiwa kurushwa mubashara na mitandao ya kijamii mikubwa 25 ya hapa nchini ikiwemo MCL digital, Mwananchi digital, Majira online , anzania online , Jamuhuri online na mingine .

“Tunawaalika watu wote waje kuona namna Jukwaa la wahariri linavyotekeleza kwa vitendo Demokrasia ,ambapo kampeni zinaendelea kistarabu ,hakuna kuchafuana na tunaamini mkutano utakua wa Amani.

Aidha Tv zilioahidi kurusha Mubashara ni TBC,ITV,zamaradTv, startimes,Cloudstv,Azam,Channel 10,Crowntv,ImmaniTv ,Jambo Tv,TEF platform na vingine vingi.

Aidha amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas,Katibu tawala mkoa Mery Makondo na mkuu wa wilaya wa Songea Kapenjama Ndile kwa ushirikiano na mapokezi mazuri ambayo yamefanikisha maandalizi hayo.