Maswali kwa ajili ya kuuza viwanja
Katika mtandao wake ameweka maswali na majibu ya kuvutia wateja wafike kununua viwanja kama ifuatavyo:-

Swali: Wapi viwanja vilipo

Jibu: Kilomita 35 Kusini mwa Tanga kwenda pwani ya Barabara ya Pangani.

Swali:
Ni jinsi gani unaweza kufika resort?

Jibu:
Kwa kutumia gari kutoka Tanga dakika 40, Mombasa (saa 3), Kilimanjaro (saa 5), Dar es Salaam (saa 5).

Swali: Viwanja vilivyoendelezwa ni vipi?

Jibu: Ekari 360 kwa ajili eneo la  gofu na ekari  200  vilivyopo ufukweni mwa bahari, ambavyo ni kwa ajili ya makazi ndani ya ekari 12,000 za zao la  mkonge na za kilomita 8 ufukwe binafsi.

Swali:
Ni viwanja vingapi vinapatikana katika eneo la makazi?

Jibu:
Kunakadiriwa kuwa na viwanja 30 katika eneo la uwanja wa gofu na viwanja vikubwa kwa ajili ya makazi 50 ambayo yanakuwa kati ya ekari 3-5 mbele ya ufukwe wa bahari.

Swali:
Kama nataka kujenga nyumba ni kiasi gani cha fedha kitakachotumika?

Jibu: Gharama za ujenzi wa nyumba, Tanzania ni dola za Marekani 40 kwa mraba wa futi moja.

Swali: Kama nitanunua kiwanja na kujenga nyumba naruhusiwa kupangisha?

Jibu: Ndiyo. Timu ya manejimenti itakusaidia kupangisha au kutoa mkataba wa kupangisha kwa watalii au watu binafsi.

Swali:
Nani atakayejenga nyumba yangu?

Jibu:
Unayo nafasi ya kununua ramani ya nyumba ya kuanzia vyumba vitatu au vinne kutoka kwa mkandarasi wetu au kuijenga mwenyewe.

Swali:
Kama nina mkandarasi wa kujenga nyumba yangu mwenyewe ni gharama kiasi gani nitatumia hadi kukamilisha nyumba?

Jibu: Gharama za ujenzi Tanzania ni dola za Marekani 40 kwa mraba wa futi moja.

Swali: Je, kuna zuio la kuunda mchoro wa ramani ya nyumba niitakayo?

Jibu:
Ndiyo. Nyumba lazima iwe aina ya ‘bungalow’ ikiwa na mapambo ya asili.

Swali: Je, naweza kununua nyumba bila kuhusisha uwanja wa gofu?

Jibu: Ndiyo unaweza kununua uwanja wa ufukwe kwa haki utakayo.