Na Mwandishi Wetu.JamhuriMedia

Wadau wa sekta ya habari wamehakikishiwa kuwa mabadiliko ya sheria ya huduma ya Sekta ya habari yanakwenda kufanyika Januari 2033.

Hayo yamesemwa leo Desemba 17, 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati wakati wa Kongamano la Kwanza la Maendeleo ya Sekta ya Habari 2022 lililofanyoka jijini Dar es Salaam.

Amesema mabadiliko hayo ni safari ya kuwezesha kulindwa kwa uhuru wa habari kwa mujibu wa sheria na sio utashi wa viongozi.

Nape ameeleza kuwa wakati hilo likisubiriwa, uhusiano baina ya sekta ya habari na sekta ya umma umeendelea kuimarika katika awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Sheria na kanuni mbalimbali zinaendelea kufanyiwa mabadiliko kwa mujibu wa sheria. Uhuru wa habari unapswa kulindwa kwa mujibu wa sheria sio utashi wa viongozi. Kiongozi yeyote atakayekuja atalazimika kuulinda uhuru huu kwa mujibu wa sheria hata kama hataki” amesema.