Namshukuru sana Rais John Magufuli kwa kurudisha uwajibikaji. Mimi ni mzee mwenye umri wa miaka 94 nikiwa miongoni mwa askari tuliopigana vita ya KAR ya mwaka 1952, namba yangu ilikuwa A.181300135. Malkia wa Uingereza alituma fedha za fidia lakini hatujalipwa hadi sasa.
Hassan Sudai, Dodoma,0742082319, 0684820477
Mhariri wa JAMHURI
Umesema ukweli Mhariri, kuna dalili zinazoashiria nchi hii kurejea katika mfumo wa chama kimoja cha siasa na vyama vya upinzani vitauawa. Mkakati wa kuvidhoofisha umeanza. Watanzania tupinge njama hizi kwa nguvu zote.
Msomaji wa JAMHURI, 0754959526
Nahitaji msaada
Naomba mtu yeyote mwenye mapenzi mema anisaidie niweze kuendelea na masomo kwani niko tayari hata kwa kuwekeana mkataba ili nirudishe mkopo huo baada ya kumaliza masomo yangu.
Magayane 0756629565
Wauguzi heshimuni wagonjwa
Kero yangu ni kwa wauguzi wa hospitali ya Ndanda, kwani hawawathamini wagonjwa, wanawaporomoshea matusi. Nimekaa katika wodi ya wazazi kwa siku sita nauguza kidonda na bandeji nilizowekewa chumba cha upasuaji hazijatolewa mpaka naruhusiwa kutoka hospitalini.
Jane James, Kanoge, 0757239761
Barabara Mwanza itengenezwe
Jiji la Mwanza lina barabara moja tu inayoingia na kutoka, lakini imejaa viraka na mabonde. Wageni wanaingia na kutoka ndani ya Jiji hili kwa kutumia barabara hiyo, inatia aibu. Serikali ijenge barabara yenye njia nne au sita kutoka Usagara hadi Nyakato kuvutia watalii.
Msomaji wa JAMHURI, Nyegezi, 0762877739
Wafanyakazi tunanyanyaswa
Sisi wafanyakazi wa hoteli ya Andbeyond, Ngongoro Crater tunanyanyaswa na mwajiri wetu. Tunamwomba Waziri mwenye dhamana ya kazi aingilie kati mgogoro huu kwani Mwenyekiti wa CHODAWU wa tawi ameachishwa kazi na Katibu amehamishiwa hoteli nyingine ili kuua chama cha kazi mahali pa kazi.
Msomaji wa JAMHURI, Arusha, 0753808890
Tatizo la maji Uru
Tatizo la maji limekuwa likisumbua baadhi ya maeneo ya Uru licha ya kuwepo kwa vyanzo vingi vya maji, bado tunasubiri ahadi ya Waziri ya utandikaji wa mabomba ili maji yawafikie wakazi wote.
Msomaji wa JAMHURI, Uru, 0762888396
Yatima na Krismasi, mwaka mpya
Kero yangu mimi ni makundi mbalimbali kuamua kuwakumbuka yatima na wasiojiweza nyakati za Krismasi na Mwaka mpya tu na kutaka kupiga picha nao ili waonekane. Je, miezi mingine kabla ya sikukuu hizo kwa nini hawatoi misaada hiyo?