Siku ya Hedhi Duniani kuazimishwa le tarehe 28/Mei/2018, huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile. Tukio hilo linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oyster bay, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Chief Promotions Bwana Amon Mkoga amesema kuwa, wataanza na matembezi maalum ya siku hiyo ya Hedhi duniani, majira ya Asubuhi ya saa 12 na baadae kumalizikia kwenye viwanja hivyo vya Polisi Oyster Bay.
“Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Hedhi duniani. Taasisi ya Chief Promotion, kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo kampuni ya Pedi za kike ya Reliefline Tanzania Limited wasambaaji na wauzaji wa Relief Pad na kampuni ya pedi za HC, HQ, kwa pamoja na wengine wataungana katika siku hii ambapo watatoa elimu ya namna ya matumizi sahihi na salama ya pedi kwa wasichana.
Katika tukio hili ya siku ya hedhi hapo kesho Mei 28, pia zitatolewa pedi ama taulo maalum za RELIEFPAD kwa Wasichana 500, ambao watapatiwa bure na pedi hizo ni maalum wanaweza kuzitumia kwa muda wa mwaka mzima, ambapo ambapo watakuwa wakizifua baada ya matumizi” alieleza Amon Mkoga.
Mkoga ameongeza kuwa, pia katika tukio hilo,Mabalozi kutoka Nchi zaidi ya sita wataungana kushiriki tukio hilo.
Kwa upande wake Meneja uzalishaji wa biashara wa Relief Line Ltd hapa nchini, Sangamesh Salmath amesema kuwa, bidhaa zao hizo ni za kisasa na ubora wa hali ya juu ambapo kwa sasa wameleta soko hilo nchini Tanzania ili kusaidia wasichana wanotoka kwenye maisha ya chini ambao hawana kipato cha uhakika.
“Pedi hizi kwa msichana atakaye zipata zitamsaidia kwani ni za kisasa na zimezingatia ubora wa hali ya juu. Mtumiaji akisha tumia anaweza kuzifua kwa matumizi ya kipindi kingine ambapo itadumu kwa muda wa mwaka mzima” alisema Sangamesh.
Nae Mwakilishi wa kampui ya pedi za HQ, Bi. Hilda Chalila amesema kuwa, HQ pads ni miongoni mwa bidhaa bora ambazao zimekuwa zikifanya vizuri na watumiaji wake wengi wamezipokea hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa tukio hilo, watatoa elimu sahihi ya matumizi ya pedi pamoja huku pia kukitarajia kuonesha na kuuza.
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bwana Amon Mkoga (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo la Siku ya Hedhi duniani ambalo linatarajiwa kuazimishwa kesho kwa kuwa na matembezi maalum ya ambayo yataanza majira ya Asubuhi ya saa 12 alfajili kwenye viwanja vya Coco Beach na baadae kumalizikia kwenye viwanja vya Polisi Oyster Bay. Kulia kwake ni Mwakilishi wa HC, HQ Pads, Bi. Hilda Chalila na kushoto ni Meneja uzalishaji wa biashara wa Relief Line Ltd hapa nchini, Sangamesh Salmath
Meneja uzalishaji wa biashara wa Relief Line Ltd hapa nchini, Sangamesh Salmath akiwa na Mkurugenzi wa Chief Promotions Bwana Amon Mkoga wakionesha aina ya pedi ambazo zitagawiwa bure hiyo kesho kwa wasichana zaidi ya 500, wakati wa tukio hilo la Siku ya Hedhi duniani ambalo linatarajiwa kuazimishwa kesho kwa kuwa na matembezi maalum ya ambayo yataanza majira ya Asubuhi ya saa 12 alfajili kwenye viwanja vya Coco Beach na baadae kumalizikia kwenye viwanja vya Polisi Oyster Bay.
Meneja uzalishaji wa biashara wa Relief Line Ltd hapa nchini, Sangamesh Salmath akitoa maelezo namna ya pedi aina ya Relief pads zinavyofanya kazi kabla na baada ya matumizi kwa waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bwana Amon Mkoga (katikati) wakionesha bana za Relief pedi ambazo kesho wtazigawa bure kwa wasichana 500, kutoka katika shule za Dar es Salaam ikiwemo Kisutu, Zanaki na zinginezo. Kulia kwake ni Mwakilishi wa HC, HQ Pads, Bi. Hilda Chalila na kushoto ni Meneja uzalishaji wa biashara wa Relief Line Ltd hapa nchini, Sangamesh Salmath