NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuonya Diwani Faustin Shibiliti wa Kata Igalula kutopotosha umma juu ya mkataba wa uwekezaji wa mnara katika kata hiyo ambapo ina minara miwili ya Vodacom na Halotel.

Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Diwani Faustin alipaswa kufika ofisi ya Mkuu wa wilaya ili kufikisha malalamiko yake.

Awali Diwani Faustin Shibilti amedai kijiji hakina mkataba na Kampuni ya Halotel kwani tangu kujengwa mnara huo hawanufaiki na chochote tofauti na Vodacom.

Mhandisi Maryprisca anaendelea na ziara zake na ndani ya wiki moja ametembelea mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Mbeya na Mwanza baadae ataelekea mkoani Mara zaidi akitekeleza agizo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la kutenganisha Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ili wizara hiyo iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuelekea uchumi wa kidijitali.