Al Ahly ya Misri wanakusudia kuvunja mkataba na mchezaji wa Afrika Kusini, Percy Tau, baada ya mchezaji huyo kupata majeraha katika mechi ya juzi kati ya Al Ahly na Ghazl Al Mahal kwenye mechi ya ligi kuu nchi Misri.
Percy Tau alikuwa na majeraha yaliyomuweka nje zaidi ya miezi mitatu na baada ya kurejea mchezaji huyo amefunga magoli mawili katika mechi mbili za mwisho huku akifunga goli moja moja kila mechi.
Mchezaji huyo wa zamani wa Brighton and Hoves ya nchini Uingereza ambaye alisajiliwa klabuni hapo raia mwenzake wa Afrika Kusini, Pitso Mosimane, amepata majeraha yatakayomlazimu kukaa nje ya uwanja Kwa miezi miwili.
Percy Tau amekuwa katika wakati mgumu kikosini hapo toka kuondoka Kwa Pitso Mosimane ambapo wadau wengi wamekuwa wakipona usajili wake kwa madai kuwa hana hadhi ya kuchezea klabu hiyo.
Hoja ya majeraha inaweza kuwa kama fimbo itakayotumiwa na mahasimu wake ambao walikataa usajili wake na ule wa Luis Miquissone aliyetokea Simba SC naye akisajiliwa na Pitso Mosimane. Luis Miquissone tayari hayupo klabuni hapo baada ya kutolewa kwa mkopo.