MZEITUNI ni mti unaostawishwa katika mataifa mbalimbali duniani. Pamoja na kupatikana kwenye nchi nyingi, lakini Israel ambayo ni nchi takatifu, ni miongoni mwa mataifa yanayostawisha kwa wingi zaidi mmea huo.

Mti huu ni ule uliotajwa mara kadhaa ndani ya vitabu vya maandiko matakatifu (Quran na Biblia). Nchi zinazozalisha kwa wingi zaidi mizeituni duniani ni Hispania ikifuatiwa na Italia, Ugiriki na Uturuki.
Una sifa za kustaajabia ukilinganisha na miti mingine tunayoifahamu. Mti huu ukikatwa mizizi yake huchomoza machipukizi mapya mara moja.

Nchini Israel mizeituni inapatikana kwenye Pwani ya uwanda wa Sharoni kwenye vilima vyenye mawemawe vya Samaria na mabonde yenye rutuba ya Galilaya.

Licha ya wakulima kutazamia faida ya mafuta kutokana na mti huo, tawi la mzeituni linatazamwa kama ishara ya wingi, utukufu na amani.
Kwenye kitabu cha Kumbukumbu la Torati, Nabii Musa amenukuliwa akiitaja Israeli kuwa nchi nzuri ya mizeituni na asali.

Aidha, hapa nchini inastawishwa kwa kiwango kidogo hivyo kuwafanya watu wengi kuwa na uelewa hafifu kuhusu mmea huo.

Katika Waamuzi 9:8 maandiko yanasema, “Siku moja, miti ilikwenda kujitafutia mfalme. Basi ikauambia mzeituni tawala juu yetu.

Pamoja na hayo yote mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai anasema mti huo ni wa ajabu kwa kuwa umebarikiwa na Mwenyezi Mungu.

Anasema katika Quran Tukufu Mungu ameutaja mzeituni katika aya nyingi mno na Mtume Muhammad (SAW) amesema kuleni mazaituni na mjipake mafuta yake kwa kuwa yanapatikana katika mti uliobarikiwa.

Aidha, mtaalamu huyo anasema si hayo tu mzeituni kama ilivyo mimea tiba mingine, unasaidia kutatua matatizo mengi ya kiafya yanayoikabili jamii katika karne hii.

Mtaalamu Mandai anasema mzeituni una faida kubwa kitiba kuanzia mizizi, matunda hadi majani.

“Tunda la mzeituni lina linasaidia kwa mtu anayekabiliwa na tatizo la kiharusi, pia linaondoa makovu katika mwili wa binadamu.

“Mafuta ya mzeituni yanasaidia kuondoa mafuta katika moyo wa binadamu na hivyo kumkinga mtumiaji na uwezekano wa kupata maradhi ya kiharusi,” anasema.

Anabainisha kuwa kwa anayekabiliwa na tatizo la maumivu ya kichwa anaweza kunyoa nywele na kisha kupaka mafuta ya mmea huu yanasaidia kumaliza tatizo hilo.

Kwa mwanamke anayenyonyesha ambaye anakabiliwa na tatizo la uhaba wa maziwa kwa ajili ya mtoto wake, anamshauri kula tunda la mzeituni litamsaidia kutokwa na maziwa ya kutosha.

“Wanawake wenye tatizo la mauamivu wakati wa hedhi, mzeituni unaweza kuwasaidia kuondokana na tatizo hilo,” anasema Mandai.

Mti huu pia ni msaada kwa wanawake wenye tatizo la kumwagika maji yenye harufu mbaya sehemu zao za uzazi, hivyo anashawauriwa kutumia juisi yake kwa kuwa inasaidia kuondoa tatizo hilo.

“Mwanamke mwenye matatizo ya kumwagika maji, anaweza kuponda majani na kuyaweka sehemu ya uzazi pamoja na pedi kwa muda fulani, yatamsaidia kuondoa tatizo hilo.

“Pia tiba hii inawasaidia kinamama wenye tatizo la fangasi aina ya kandida, watumie majani ya mtii huu kama wale wenye tatizo la kumwaga maji,” anabainisha.

Mti huo ambao unaweza kuishi zaidi ya miaka 1,000, Mandai anasema unasaidia pia kwa wazee wanaosumbuliwa na maumivu ya miguu na kufa nganzi anawashauri waichue kwa kutumia mafuta ya mzeituni wanaweza kupata nafuu.

Mandai anaongeza kuwa mizizi ya mzeituni pia ikichemshwa na maji yake kunywewa inasaidia kwa anayesumbuliwa na maradhi ya figo, kwa kuwa ina nguvu ya kuondoa kemikali katika kiungo hicho ambacho ni miongoni mwa vilivyo muhimu katika mwili wa binadamu.

Mtaalamu huyo mwenye kituo chake cha ushauri wa mambo ya kiafya ambacho pia kinazalisha virutubisho asilia, anasema mzeituni ni moja ya mimea anayochanganya kupata virutubisho hivyo ambavyo pamoja na mambo mengine vinasaidia kumwondolea uchovu wa mwili mtumiaji.

Katika chake hicho kilichoko Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam, mtaalamu Mandai anatoa mwito mwa wenye changamoto za kiafya kwenda kupata ushauri na virutubisho vyenye nguvu ya kuondoa uchovu na changamoto nyingine za kiafya.

Anabainisha kuwa mmea huo ni ule ambao mara nyingi waandishi wa maandiko matakatifu wameutumia kama mfano katika sehemu mbalimbali za mandiko yao kuufananisha na rehema za Mungu, ahadi ya ufufuo, na maisha ya familia yenye furaha.

“Mafuta ya mzetuni pia ni tiba mujarabu kwa kina baba wanaokabiliwa na tatizo la nguvu za kiume, kijiko kimoja cha mafuta hayo wachanganye na kitunguu swaumu, wanywe mara moja kwa siku muda wa siku saba hadi 11 kisha wapake sehemu zao za uzazi watarudisha heshima yao.

“Pia kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku cha mafuta haya muda wa siku saba hadi 14 kunasaidia kuua wadudu wabaya wa tumboni,” anasema mtaalamu huyo.

Aidha, mafuta haya ni msaada kwa wenye tatizo la vidonda vya tumbo, watumie vijiko viwili vya chakula katika uji kila siku, wafanye hivyo kwa muda wa siku 90 wataondokana na tatizo hilo.

Mandai ambaye anatoa huduma zake kwa kutumia virutubisho asilia, anatoa mwito kwa watu wenye changamoto mbalimbali za kiafya kwenda katika kituo chake watanufaidiaka na huduma za ushauri wake wa namna ya kuepuka magonjwa mbalimbali kwa kuzingatia kula lishe bora.

Anasema ana amini kuwa jamii ikiwa na uelewa mzuri wa namna ya kupangilia mlo inaweza kuepukana na magonjwa mbalimbali kwani mengi yanatokana na ulaji chakula usiozingatia kanuni.

Mandai anatoa mwito kwa Watanzania kupanda mti huo na mingine kwa wingi katika mazingira wanayoishi ili kutunza mazingira, lakini pia watapata matunda na dawa kwa ajili ya miili yao.

Please follow and like us:
Pin Share