Rais Kikwete (kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na waombolezaji wengine msibani hapo.
Mwili wa marehemu ukishushwa kwenye gari makaburini hapo.
Rais Mstaafu ya Awamu ya Nne Dr. Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mpiga picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi katika maziko yaliyofanyika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo , Dr Harison Mwakyembe akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mpiga picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi katika maziko yaliyofanyika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
Rais Mstaafu ya Awamu ya Nne Dr. Jakaya Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo , Dr Harison Mwakyembe katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam
Waombolezaji wakihuhifadhi mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi
Waombolezaji wakiusaliwa Mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi katika Msikiti wa Sinza Madukani
Mwenyekiti wa Chama cha Wapigapicha za Habari nchini, Mwanzo Milinga akiweka Udongo kwenye kaburi la aliykeuwa mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu , Gerson Msigwa akiweka Udongo kwenye Kaburi la aliyekuwa mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Serikali Athumani Hamisi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwa Marehemu Athumani Hamisi Sinza Madukani Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiteta na Katibu wa Chama cha wapigapicha za Habari nchini Tanzania , Mroki Mroki nyumbani kwa Marehemu Athumani Hamisi Sinza Madukani Jijini Dar es Salaam
Wanahabari na waombolezaji wakiwa makaburini kwa ajiri ya maziko hayo
Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akisalimiana na waombolezaji.
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete ameongoza mamia ya wananchi wa Dar es Salaam katika mazishi ya aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa magazeti ya Serikali ya Habari Leo na Daily News Athuman Hamis yaliyofanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete katika mazishi hayo alikuwa ameongozana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harson Mwakyembe, Viongozi wa Serikali, Wahariri, wanaandishi wa habari pamoja na wapiga picha za habari katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Mauti ya mpigapicha huyo yalimkuta jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kabla ya mazishi hayo, nyumbani kwa marehemu Athumani Hamis Sinza Madukani , Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya TSN, Dk.Jim Yonas amesema, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mbali ya kuguswa na kifo cha Athuman Hamis pia ameahidi kuijengea nyumba familia ya marehemu itakayokuwa na vyumba vinne.
“Nilikuwa nazungumza na Mkuu wa Mkoa wetu wa Dar es Salaam na ameniambia kuwa ofisi yake itajenga nyumba ya vyumba vine kwa ajili ya familia ya marehemu Athuman Hamis,”amesema Dk Yonas.
Pia amemueleza marehemu Hamis kuwa enzi za uhai wake alikuwa mchapakazi hodari na licha ya kuwa na matatizo ya kiafya bado aliipenda kazi yake.
Amesema Athuman Hamis ameacha pengo kubwa katika tasnia ya habari na kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake hasa kwa wapiga picha wa vyombo vya habari nchini.Akizungumza baada ya kumzika marehemu Hamis , Imamu wa Msikiti wa Sinza Maijiku Sheikh Mohamed Suileman amesema enzi za uhai wake Hamis alikuwa ni mcha Mungu na alipenda kufanya ibada.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema Athuman Hamis wakati wa uhai wake kabla ya kupata kupata matatizo ya ajali alikuwa ni mtu mwenye kupenda kufanya ibada.
Post Views: 324