RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, mapema leo ameungana na baadhi ya wapenzi na wanachama wa Klabu ya Yanga kuuzika mwili wa aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Athumani Chama kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbali na Kikwete maziko hayo pia yamehudhuriwa na baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wao Clement Sanga na viongozi wa Serikali ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba alihudhuria.