Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk Rose Rwakatare, amehitimisha ziara yake mkoani humo akiwataka viongozi kuhakikisha wanaanzisha miradi ya kiuchumi ya Jumuiya.
Dk. Rose amesema kila Wilaya ihakikishe inakuwa na nyumba za watumishi wa Jumuiya hiyo na kusisitiza umoja na mshikamano ndani ya Jumuiya hiyo.
Akizungumza wakati akihitimisha ziara hiyo Morogoro Mjini, Dk. Rose aliwaasa wazazi kusimamia maadili mema katika jamii na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na matumizi ya dawa za kulevya.
Alitembelea watu wenye mahitaji maalum kuwafariji kwa kuwapa baadhi ya mahitaji mbalimbali na kuiasa jamii kujenga utamaduni wa kutembelea familia zenye mahitaji ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali .
Dk. Rose alisisitiza uhai wa chama na Jumuiya ya Wazazi na alikagua miradi mbalimbali ya Jumuiya na serikali huku akisisitiza viongozi kujitahidi kutatua baadhi ya changamoto zinaikabili Jumuiya hiyo .
Mwenyekiti huyo pia alikagua miradi ya ufugaji wa kuku na ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Gairo na Wilaya kilombero na kuahidi kuwa atasaidia ujenzi wa nyumba hizo.
Dk. Rose pian aliahidi kuchangia mifuko ya saruji katika ujenzi wa Zahati ya Ipopoo na kuwapatia taulo za kike wanafunzi wa ya sekondari Miembeni Wilaya ya Malinyi.
Katika ziara hiyo, Dk Rose alikagua mradi wa shamba la mikorosho na kuchangia pesa kwaajili yakununua kiwanja cha ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini na kutembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kufugia samaki.
Kutokana na changamoto ya usajili wa wanachama wapya wa Jumiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro, Dk. Rose aliwakakadhi kadi 500 za Jumuiya ya Wazazi kwa kila Wilaya na kuwaelekeza viongozi wa Jumuiya wa Wilaya hizo kuhakisha wanaongeza idadi ya wanachama wasiopungua 100 kwa mwezi.
Dk Rose alihamasisha umuhimu wa michezo kwa kutoa vifaa ya michezo wilaya zote alizotembelea ikiwemo jezi na mipira ya miguu ili wawezekuanzisha ligi katika wilaya zao na kutumia fursa hiyo kupata wanachama wapya wa jumuiya ya wazazi.