Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Zanzibar
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Tanzania , Dk Samia Suluhu Hassan amemwagia sifa Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya CCM, Issa Haji Gavu.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja, Mwenyekiti Dk Samia amesema Gavu ameiweza idara utendaji wake ni wa kupigiwa mfano na ameiweza idara anayoiongoza.
“Ndugu Gavu ameiweza Idara ya oganaizesheni naomba awasalimie,” alisema Dk Samia.
Katika kipindi kifupi cha uongozi wake katika Idara hiyo, Gavu ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka, Mkoa Kusini Ungua, amefanya mageuzi makubwa kimfumo ndani ya idara hiyo muhimu, ambayo ndiyo injini katika mustakabali wa ushindi wa CCM..
Awali akizungumza katika mkutano huo, Gavu amemuhakikishia Mwenyekiti wa CCM Taifa kuwa kwa Mkoa wa Kusini Unguja ushindi wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 hautapungua asilimia 90.
Amesema Mkoa wa Kusini umepiga hatua kubwa za maendeleo, akitolea mfano miaka miaka kumi au 20 iliyopita haikuwa ilivyo leo, hivyo wana CCM katika Mkoa huo, wana deni kubwa la kuilipa CCM kwa kuiletea ushindi usiopungua asilimia 90.
Gavu alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika uongozi wa Serikali ya awamu ya saba Zanzibar iliyoongozwa na Dk Ali Mohamed Shein.