Na Helena Magabe, JamhuriMedia, Tarime

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Mkoa wa Mara (BAWACHA), Veronica Irecho amekemea vikali vitendo vya rushwa vinavyojitokeza ndani ya Chama cha Demokakrasia na maendeleo (CHADEMA)

Akizungumza katika kikao cha 7 tangu aanze ziara ya kuhamasisha uhai wa BAWACHA Majimboni kilichofanyika katika ofisi ya chadema Tarime mjini amesema lengo ni kuhamasisha wanawake kujiandikisha kupiga kura,kugombea nafasi mbali mbali sambamba na kukemea vitendo vya rushwa ndani ya chama.

Ikiwa ni mara ya kwanza kukutana na wajumbe wa Bawacha wa Tarime amekemea vikali vitendo vya rushwa ndani ya chama ambapo amewataka wanawake kuepuka rushwa kwani ni mbaya itapelekea kukosa nafasi mbali mbali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 pamoja na Serikali kuu 2025.

Irecho ambaye ni Diwani Mstaafu wa viti maalumu pia amechangia mifuko mitano ya saruji kwa ajili ya ofisi ya chama na kusema Chadema ni cha kuchangishana na kujitolea na mambo yanaenda sawa lakini kwa sasa anasikitika kuona yale ambayo yalikuwa yakilalamikiwa kwenye baadhi ya vyama kwa sasa ndiyo yako Chadema, kwani wanachama wakiitwa kwenye vikao wanaanza kuhoji juu ya kulipwa posho na mengineyo ambayo hayafai kwenye chama chao.

“Chukueni fomu mjaze kwa hiyari mkishinda tumikieni Taifa acheni tamaa ni mbaya kemeeni huyo shetani wa rushwa aliyewavagaa taama huzaa dhambi jimboni kwangu pia kuna hiyo shida mtu akiitwa anaanza kuhoji atatupa nini atatulipa posho fanyeni kazi kama mlikuwa mmelala muamke vinginevyo mjiandae kuniona adui ntakuwa mkali” alisema Irecho.

Aidha amesema kikao kingine cha Jimbo la Tarime vijijini kitakuwa Julai 17 katika ofisi ya Tarime mjini kikihusisha maswala kama hayo hayo huku akisisitiza wanawake kuwa mstari wa mbele kupinga rushwa ndani ya chama huku akiahidi kutumia wadau pamoja na wakufunzi kwenye chama kuwapa semina wanawake hoja iliyotolewa na mjumbe Prisca Hassan kuwa wanawake wa wapigwe msasa kujengewa uwezo.

Mwenyekiti wa Kanda Lucas Ngoto amesema Biblia inasema wanawake ni jeshi kubwa hivyo wasaidie Chadema kuingia madarakani sio kwa kugombea tu bali kwa kutoa maoni ni nani anafaa kugombea Serikali za Mitaa na anayefaa kugombea Serikali Kuu na wasikubali kiongozi yoyote kuwadanganya kuwapa viti maalumu huyo ni tapeli.

Amesema lazima chama kiweke utaratibu wa kutokomeza rushwa nakuwepo nidhamu kwani kukosekana maadili sio kwa vijana pekee au wazee wapo kina mama ambao hawana breki juu ya kipi waongee hivyo ameonya vikali kuwa chama cha Chadema ni lazimiza kiwe na msingi imara wa maadili.

Kwa upande mwingine wamejitokeza watia nia wawili wa kugombea ubunge Jimbo la Tarime mjini ambao ni Esther Nyabulili, pamoja na Rejina Mbusha ambaye ni Mjumbe wa Bawacha Mkoa.

Hata hivyo mtia nia mwingine aliyehudhuria ayeungana na Bawacha kwenye kikao chao Bob Zakayo Wangwe ambaye ni mwanasheria amewatia moyo kina Mama Wajane waliopoteza waume zao hifadhini na mgodini,na wale ambao watoto wao wamepotezwa ambapo amewambia ameunganisha Voice of America kufanya uchunguzi na tayari wameanza kufanya tafti kubaini kinachofanyika.

Please follow and like us:
Pin Share