Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 zimewasili mkoani Geita kutokea mkoani Shinyanga ambapo utakimbizwa katika halmashauri sita, kutembelea, kukagua na kuzindua miradi 59 yenye thamani ya Sh bilioni 24.2.

Akizungumuza wakati wa mapokezi ya mwenge katika kijiji cha Nyang’olongo wilayani Nyang’hwale, leo Agosti 2, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani hapa utakimbizwa Km 755.54.

Amefafanua, viongozi wa mbio za mwenge wanatarajia kufungua miradi mitatu, kuzindua miradi 21, kukagua miradi 22 na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 13.

Amesema kwa kuzingatia ujumbe wa mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2023, usemao Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai na kwa Ustawi wa Uchumi mkoa umetekeleza miradi tofauti ikiwemo upandaji miti.

Shigela amesema kwa mwaka 2022/23 mkoa umepanda jumla ya miti milioni 5.07, uhamasishaji wa matumizi ya nishati mbadala kwa taasisi na wananchi na utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya usafi mwisho wa mwezi.

Amesema pia mkoa unaendelea kuunga mkono juhudi za kitaifa za kupamabana na maambukizi ya viruisi vya ukiwmi ambapoo mkoa umepunguza Kasi ya maambukizi ya hadi kufikia asilimia tano kwa utafiti wa mwaka 2016).

Amesema pia takwimu za upimaji zinaonesha kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 waliopimwa UKIMWI katika Mkoa wa Geita ni watu 436,031.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023, Abdullah Shaibu Karimu amesisitiza watapitia miradi husika kujiridhisha ubora na thamani halisi ya miradi na utekelezaji wa kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2023.