Franone Mining yavunja rekodi na kuishangaza Serikali
Waziri wa Madini Dkt.Dotto Biteko amemshuruku Rais Samia Suluhu Hassan juu ya uamuzi wake wa Mgodi wa Madini ya Tanzanite ‘ Kitalu C ‘ cha kumpata Mwekezaji mzawa na Mtanzania wa Kampuni ya Franone Mining Onesmo Mbise ambaye anafanya vizuri, aliyeanza kuzalisha madini ndani ya miezi 6 badala ya 18
Hayo yamebainishwa na Dkt. Biteko wakati akikagua maendeleo ya Mgodi wa Kitalu C, na ujenzi wa Jengo la soko la Madini ya Tanzanite katika eneo la Mirerani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Dkt.Biteko amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uamuzi sahihi juu ya Kitalu C, kwani wapo waliodhani kuwa Serikali ilikurupuka tu likaibuka juu uamuzi wa kitalu C kutafutiwa Mwekezaji na Rais Samia akaenda mbali zaidi akasema huyo Mwekezaji lazima awe mzawa na ni Mtanzania.
” Tunashukuru kwamba leo kwa mara ya kwanza tumekuja hapa tumekuta kuna hatua kubwa imepigwa na mipango mingi imefanyika, tumepata Mwekezaji anaitwa Franone Mining Mmiliki wake ni Onesmo Anderson Mbise , alituambia na kwenye mkataba wake na Serikali kwamba ataanza uzalishaji miezi 18 baada ya kupatiwa leseni, mwema huyu amepambana ndani ya miezi 6 ameanza uzalishaji” amesema Dkt.Biteko.
Aidha amesema Mgipodi huo ulikua umechakaa Onesmo ameweka uwekezaji mkubwa, amekarabati, tayari ameahidi watu 328, watu ambao hawakua nankazi kipindi kilichopita, ambapo muda huo mfupi ambapo Wizara tuliaminmwekezaji bado yuko kwenye Ujenzi wa miundombinu, ameshafanya uzalishaji na tayari Madini yamepelekwa kwenye masoko na fedha zimekusanywa kama Serikali.
” Tunakusanya Kodi kwenye ajira ya watu hawa 328, na tunakusanya kodi kwenye Madini, ni Mtanzania ambaye anatupa heshima kubwa Watanzania, huyu bwana ameleta heshima kunpbwa kwenye Sekta hii ya Madini ya Tanzanite na sis kama serikali tunamuunga mkono” amesema Dkt.Biteko.
” Tulipowatembelea Kikundi cha akina mama wanaotengeneza kamba mmoja ameongeza jambo limeniuma sana amesema nenda tupelekee salamu Kwa Rais Samia kuwa tunamshukuru kwa kutuletea mwekezaji zawa na Mtanzania, mngelea mgeni mimi sijui kizungu nisingeajiriwa hapa, Lani mwambie Mama Samia ameleta Mtanzania mwenzetu hata kimasai tunazungumza naye nanhata mshahara anatupa tena Kwa wakati bila kuchelewala” alifafanua Dkt.Biteko.
Aidha aliwatahadhalisha watu kuwa wengi wamekua wakiaminimkuwa ili mtu awe Mwekezaji ni lazima asiwe mweusi , awe mgeni kutoka mbali, ambapo alisema ni vema watu wakaondokana na hiyo imani potofu Onesmo Anderson Mbise ni mzawa na Mtanzania anayefanya vizuri ndani ya Kampuni yake ya Franone Mining na ndio maana Serikali ikamuanini na kumkabidhi Kitalu C huku Serikali nayo ikiwa na asilimia 16 ya hisa.
” Kwenye Mgodi huu wa Kitalu C Franone Mining haiko peke yake, Serikali imo nayo inamiliki asilimia 16, hivyo ni vema Watanzania wakatambua hili vizurinili iuepuka Hali yanupotoshaji, ambapo amewataka Watanzania kuweza kumuunga mkono mwezaji mzawa” ameongeza Dkt.Biteko.
Naye Meneja Mkuu na Mtaalam wa Miamba wa Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd Vitus Ndakize amesema Kampuni tangu iliposhinda hiyo tenda ya kuchikba Kitalu C miezi 5 iliyopita wameweza kukarabati Mgodi nankutengeneza ajira zisizo rasmi 1000.
” Walioajiriwa moja kwa moja na Kampuni ya Franone Mining ni watumishi 328, kati yao 30 ni Wataalam mbalimbali wanaohusika ndani ya uendeshajinwa Mgodi hu, waliobaki wote ni wafanyakazi wachimbaji ” amesema Ndakize.
Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini Mirerani Menard Msengi, amesema kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 ofisi yake imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.6 sawa na asilimia 52 .2 3 ya lengo la makusanyo huku akieleza sababu zilizosababisha baadhi ya malengo kutofikiwa ni pamoja na hali ya kijiolojia ya mashapo kuwa katika kina kirefu hivyo migodi mingi kutumia muda mrefu kufanya utanuzi na uwekezaji wa migodi pamoja na ukosefu wa teknolojia za kisasa kwa wachimbaji wadogo ndani ya eneo la ukuta.
Maengi pia amebainisha baadhi ya changamoto zilizopo katika eneo hilo la Mirerani kuwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za kijamii yaani maji Safi na salama, umeme na ukosefu wa mawasiliano katika baadhi ya maeneo ya uchimbaji wa Madini.
Aidha ameeleza mikakati waliojiwekea ni kuongeza vituo vya madini ujenzi kwa ajili ya kupata wadau wengi wanaofanya biashara ya madini ujenzi hasa ya mchanga na kokoto na ufuatiliaji wa karibu wa miradi inayorajiwa kuanzishwa muda si mrefu wa madini ya Kinywe yaliopo karibu la eneo la Mirerani.