Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha
Arusha .MWANASHERIA Mkuu wa serikali Hamza Johari amewataka Wanasheria na Mawakili wa serikali kuhakikisha wanatoa huduma zao kwa wakati na kuzingatia weledi na ubora ili wateja waweze kupata huduma kwa wakati.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akizungumza katika.mafunzo ya siku tano kwa Wanasheria na Mawakili wa serikali kutoka mikoa mbalimbali .
Amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kunakuwepo na ubora kwenye swala la sheria ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa ubora bila kuchelewachelewa kwani bila kufanya hivyo wanaathiri uchumi wa nchi.

“Tunataka kuona wanafanya kazi kwa kasi na ubora na kwa weledi mkubwa ili kuwa na nchi ya uchumi yenye viwango vya juu,tuwe mfano wa kuigwa tufanye kazi katika kasi inayostahili.”amesema Mwanasheria Mkuu .
“Tunataka kuona wanafanya kazi zao kwa haraka na kwa wakati na huduma wanayoletewa wafanye kwa wakati wasipofanya hivyo watakuwa na ugonjwa wa kufanya kazi kwa kuchelewa na hivyo wateja kukosa huduma kwa wakati na kuathiri uchumi wa nchi na naomba mhakikishe mnafanya kila jambo kwa wakati na kuzingatia ubora “. amesema.
Amesema kuwa, wanaongeza umahiri katika sekta ya Sheria kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa ubora na kwa haraka bila kuchelewa .
“Wafanye kazi kwa haraka na kwa ubora wasicheleweshe kazi kwani itahadhiri uchumi wa nchi hivyo ni vizuri wakafanya kazi kwa ubora na weledi ili Taifa liweze kuwa la uchumi wa kati na kuwa mfano wa kuigwa .”amesema .
Ameongeza kuwa,Sekta ya Sheria ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya Taifa hakuna kitu kitafanyika bila kuwa na Sheria mahususi katika sekta mbalimbali ambapo amesema kuwa Sheria hizo zikaandikwa vizuri itasaidia ukuaji wa uchumi.
“Mikataba yote inayotekelezwa kwenye miradi mbalimbali inaandikwa na sisi wanasheria hiyo mikataba lazima iandikwe vizuri. “amesema .

Amefafanua kuwa, wamejipanga kuhakikisha mikataba wanayoingia wanaingia vizuri na Sheria zinaandikwa vizuri kwa maslahi ya nchi yetu.
Kwa upande wake Jaji mstaafu Sirilius Mafupa amewataka wanasheria na mawakili wa serikali kuwa weledi katika uwasilishaji wa mashauri yao.
Amewataka kuwa mahiri wa sheria na weledi mkubwa huku wakijitahidi kutotumia lugha ambayo itamfanya mtu ashindwe kuelewa ushauri wake .
Naye Mwandishi Mkuu wa sheria msaidizi na Mratibu wa mafunzo haya ,Rehema Katunga amesema kuwa , mwanasheria mkuu wa serikali wana jukumu la kushauri serikali katika maswala ya kisheria mikataba kuhusu maswala ya manunuzi na uandishi wa sheria ,sheria mpya zinazotungwa na mambo mbalimbali yanayohusisha shughuli za serikali.
Ameongeza kuwa, utekelezaji wa majukumu.hayo pamoja na kuwa imekuwa ikifanyika vizuri bado kuna changamoto mbalimbali ikiwemo mikataba ambayo inafika hatua inavunjwa kwa kutosimamiwa vizuri , hivyo wanataka kuongeza umahiri kwa wanasheria na mawakili wao ili kuondoa changamoto hizo ambazo serikali inapitia.

Rehema ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga zaidi kuwapa ujuzi katika kazi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa wanapata fursa ya kutosha na kupata uzoefu zaidi .
“Washiriki wametoka sehemu mbalimbali na kuna wengine wanakosa ile fursa ya kupata mafunzo kama haya kwenye mambo yenye changamoto hivyo wakipata uelewa katika maeneo mbalimbali itawasaidia sana kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao wa kila siku ‘amesema .
Amefafanua kuwa,kupitia mafunzo haya wanasheria wote wanapata kujifunza maswala mbalimbali kuanzia majadiliano ya mikataba,usimamizi wa mikataba ,kutoa ushauri wa kisheria kwa hiyo wanapokuja hapa wanapata uelewa kuhusu maeneo hayo.
Amesema kuwa, uwepo wa mafunzo hayo yanasaidia kuandaliwa kwa Sheria bora ambazo zinaleta tija wakati wa utekelezaji .