Luis Posada Carriles, mzaliwa wa Cuba na ajenti za zamani wa CIA ambaye alitumia miaka yake mingi akijaribu kuipindua serikali ya kikomunisti ya Cuba amefarikia huko Florida akiwa na miaka 90.

Bw Posada Carriles alikuwa mmoja wa maadui wakubwa wa rais wa zamani wa Cuba Fidel Casto.

Alishiriki katika uvamizi ulioungwa mkono na Marekani mwaka 1961 na analaumiwa kwa kuiangusha ndege ya abiria.

Huku akitajwa kuwa gaidi nchini Cuba alionekana kama shujaa miongoni mwa raia wengi wa Cuba waliokuwa uhamishoni.

Wakili wake alisema Bw Posada Carriles alifarikiaakiwa makao ya wazee huko Miramar Florida baada ya kuugua saratani ya koo.

Alizaliwa nchini Cuba mwaka 1928 na kukikimbia kisiwa hicho baada ya mapinduzi ya kikomusti ambayo yalimweka madarakani Fidel Castro.

Mwandishi wa BBC nchini Cuba anasema Bw Posada Carriles alikuwa mtu aliyechukiwa sana nchini Cuba kwa kuhusika katika kuilipua ndege ya abiria ya Cuba mwaka 1976.

Watu wote 73 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliuawa wakatiandege hiyo ililipuka pwani ya Barbados.

Wakati wa kuangunshwa ndege hiyo Bw Posada Carriles alikuwa akiishi nchini Venezuela ambapo alikuwa akifanya kazi kama jasusi katika idara ya ujasusi ya Venezuela.

Uchunguzi wa kimataifa uligundua kuwa Bw Posada Carriles alipanga kulipuliwa ndege hiyo wa Cuba lakini mahakama ya kijeshi ikamuondolea mashtaka.

Hata hivyo alifungwa jela akisubiri kushtakiwa katika mahakama ya kiraia lakini akatoroka jela mwaka 1985 na kusafiri kwenda Amerika ya Kati ambapo aliendelea na mapambano dhidi ya serikali za mrengo wa kushoto huko Amerika Kusini,.

Kwa miaka mingi alipata maadui wengine na mwaka 1990 mtu alimpiga risasi kwenye na kifuani nchini Guatemala.