Katibu  wa Itikadi na Uenezi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole, ameongoza mamia ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanahabari, Justine Limonga iliyofanyika Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam leo mchana.
 
Akizungumza katika ibada hiyo, Polepole alisema CCM na tasnia ya habari imepoteza mtu muhimu ambaye alikuwa bado akitegemewa.
 
“Tumempoteza mtu muhimu ambaye alikuwa akitegemewa kama chama tutaangalia namna ya kuisaidia familia yake,” alisema Polepole.
 
Mkurugenzi wa Nduvini Auto Garage, Alhaji Ahmed Msangi alizungumza jinsi alivyomfahamu marehemu ambapo aliahidi kampuni yake kwa kipindi hiki cha kufunguliwa kwa shule itawanunulia vifaa vya shule, sare na kuwalipia karo wakati wakisubiri kukaa na familia kuona namna ya kuwazesha watoto hao kielimu.
 
Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali alisema kifo cha mwanahabari huyo aliyekuwa mwajiriwa wao kimeacha pengo kubwa ambalo halitazibika.
 Waombolezaji na wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari wa Uhuru FM, Justine Limonga wakati ukiwasili Viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa kabla ya kufanyika mazishi yake Makaburi ya Saku yaliyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.
 Katibu  wa Itikadi na Uenezi  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamphrey Polepole, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la mwanahabari, Justine Limonga.
 Waombolezaji wakisubiri kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu kwenda eneo maalumu ilipo kufanyika ibada hiyo.
 Familia ya marehemu ikiwa kwenye ibada hiyo.
 Kwaya ya Mtakatifu Kizito ya Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani, ikitoa burudani.
 Katekista wa Parokia ya Kutukuka kwa Msalaba Kizuiani,  Philo Mbunda, akitoa mahubiri.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.