Jeshi la Polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumdhalilisha kimwili na kumsababishia kifo, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU), Rahel Mkumbwa.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia Desemba12, 2024 katika mtaa wa Makorongoni, mkoani Iringa.

Akielezea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, amesema watuhumiwa walivamia chumba alichokuwa akiishi Rahel na kutekeleza ukatili huo.

Baba mzazi wa Rahel, Bw. Dickson Mkumbwa, ameomba serikali kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuhakikisha watuhumiwa wanachukuliwa hatua kali za kisheria.

Jeshi la polisi limesema kuwa chunguzi wa tukio hilo unaendelea na utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.