Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Simiyu, Latifa Juma ,17, aliyepoteza maisha kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio chumbani kwake umezikwa leo.

Tukio hilo limetokea Februari 30, 2025 na kugundulika na mama yake mzazi majira ya asubuni baada ya kumkuta amejining’iniza wakati akienda kumuamsha ili ajiandae kwenda shule.

Baba wa marehemu Jumanne Juma anayeishi mtaa wa Bariadi maarufu Mji wa Zamani ameelezea namna alivypokea taarifa hizo za msiba wa binti yake amesema: “baada ya kusikia taarifa za msiba kidogo nichanganyikiwe kwasababu nilikuwa sijielewi, kwamba ‘mtoto wako amejinyonga’ kivipi? sikufahamu jibu ni nini, kila nikiuliza siambiwi jibu na kweli hawajui kwasababu alikuwa amejifungia ndani kwake,”

Ameendelea kusema: “Askari walivyokuja walibomoa mlango na tulimkuta amejining’iniza, tukamchukua tukampeleka mochwari”

Pamoja na hayo baba wa merehemu Latifa ametoa wito kwa jamii kuwa wasiige tabia hiyo, na endapo wakipata tatizo wahakikishe wanawashirikisha wazazi wao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bariadi, Said Mapesa amewataka watoto kuzungumza na wazazi na wazazi kuwa karibu na watoto wao.