Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mwanza

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Paul Joseph (26), mwalimu wakujitolea katika Shule ya Msingi Nyang’omango iliyoko Kata ya Ntende Wilaya ya Misungwi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake.

Hayo yamebainishwa Desemba 30, 2024 na Kamanda wa Polisi mkoani humo Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Wilbroad Mutafungwa wakati akitoa taarifa za matukio mbalimbali kwa waandishi wa habari.

Alisema mwanafunzi huyo wa darasa la sita (13) ambaye jina lake limehifadhiwa alifanyiwa tukio hilo Desemba 23, mwaka huu, wakati akiwa anajisomea masomo ya ziada katika chumba cha maktaba ya shule hiyo.