Na Isri Mohamed

Bondia Hassan Mwakinyo ametembelea soko la Kariakoo katika eneo lililopata maafa ya ghorofa kuporomoka na kujionea hali halisi ilivyo.

Mwakinyo ametembelea usiku wa kuamkia leo ambapo mbali ametoa msaada ya kushuka chini ya jingo na kuongeza nguvu katika zoezi la uokoaji.

“Unajua unaweza kuchangia maji, chakula, maziwa lakini bado havina nguvu kama nguvu inayohitajika kwahiyo niliamua kufika eneo la tukio nione hali halisi na nimeshiriki kwa kadri nilivyoweza kuhakikisha na mimi natoa hisani yangu kwa watu kwa sababu miongoni mwa watu waliopoteza maisha na waliopo katika hili janga kuna watu ambao kwenye mafanikio yangu kwa namna Fulani kuna mchango wao, kwahiyo nimeona kama mpambanaji ninayo nafasi na nguvu ya kufanya”

“Inapotokea mambo kama haya ambayo yana husisha hisia, huzuni na kugharimu maisha ya watu wengine na ni janga la taifa kwa sababu ni kitu ambacho hakikupangwa, nafikiri watu ambao tuko kwenye tasnia, vioo na macho ya watu tunapaswa kujitoa kufanya vitu kwa ajili ya watu, hususani kwenye matatizo ndio wakati mzuri wa kushikana”

Aidha Mwakinyo amesema amesikia sauti za watu waliopo chini wakiomba msaada, ambapo amelipongeza jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kuhakikisha wanawafikia na kuwaokoa wakiwa salama.