Mwili wa Rachel Mkumbwa umezikwa katika kijiji cha Isongole kilichopo Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, baada ya kudaiwa kubakwa na kuuawa mkoani Iringa.

Rachel alikuwa akisoma mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu) mkoani Iringa, alikutwa amefariki dunia nyumbani kwake Desemba 12, 2024.

Baba mzazi wa marehemu Rachel Mkumbwa, Bw.Dickson Mkumbwa Mkumbwa akizungumzia tukio la kifo cha mwanae mbele ya umati wa wananchi waliojitokeza katika msiba huo

Akizungumza baada ya binti yake kuzikwa, baba mzazi wa binti huyo Dickson Mkumbwa Mkumbwa amesema licha ya mwanawe kuzikwa, anaomba serikali kupitia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kuwabaini na kuwakamata wahusika wote ili sheria ifuate mkondo wake.

Amesema unyama aliofanyiwa hauvumiliki kwani alikuwa akiishi kwa kumtumikia Mungu, lakini amefariki katika mazingira ambayo hayastahimiliki katika jamii.

Kwa upande wake polisi kata katika kata ya Isongole wilayani Ileje katika amewataka ndugu na jamii nzima kuliamini na kuliachia jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo.