Na Isri mohamed
SAA chache baada ya kutangazwa kwa kifo cha Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, aliyekuwa makamu wa Rais wake Muhammad Mukhbar anajiandaa kuiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha mpito cha siku 50.
Kwa sasa Mukhbar anasubiri tu kuthibitishwa na kiongozi mkuu wa Taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei, ili kukabidhiwa kiti hicho.
Kwa mujibu wa katiba ya Iran, Rais mpya wa Taifa hilo ni lazima achaguliwe ndani ya kipindi cha siku 50 tangu kutokea kwa kifo cha Rais aliyekuwa madarakani.