*Wasira, January Makamba, Lukuvi waongoza

*Mikakati ya kumwangushya Membe yakwama

Uchaguzi wa wajumbe 10 wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, umeshuhudia vigogo wakiibuka washindi huku Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, akiponea tundu la sindano.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, ndiye mwanamke pekee aliyeweza kupenya kwenye kundi hilo; akiwa miongoni mwa wagombea 31 kutoka Bara.


Matokeo na idadi ya kura za washindi kwenye mabano ni Stephen Wassira (2,135), January Makamba (2,093), Mwigulu Nchemba (1,967), Martine Shigela (1,824), William Lukuvi (1,805), Bernard Membe (1,455), David Mathayo (1,414), Jackson Msome (1,207), Wilson Mukama (1,174), na Fenella Mukangara (984).


Walioshindwa ni Otieno Baraka; Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji; Twalhata Ally; Godwin Kunambi; William Malecela; Salehe Mhando; Innocent Nsena; Hiza Tambwe; Anna Magowa; Christopher Mullemwah; Mwanamanga Mwaduga na Ruth Msafiri.


Wengine ni Hadija Faraji; Dk. Hussein Hassan; Nicholaus Haule; Nussura Nzowa; Dk. Kesi Mtambo; Fadhili Nkurlu; Tumsifu Mwasamale; Assumpter Mshama (Mbunge wa Nkenge) na Rashid Kakozi.


Kwa upande wa Zanzibar, wagombea 28 waliochuana ili wapatikane wajumbe 10 ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Iddi, Kidawa Hamid Saleh, Samia Suluhu Hassan, Abdulsalaam Issa Khatibu, Muhammed Seif Khatib, Khadija Hassan Aboud, Abdalla Ali Hassan na Dk. Hussein Ali Mwinyi.


Wengine ni Dk. Abdullah Juma Saadala, Mohamed Ahmada Salum, Abdulhakim Chasama, Ali Mohamed Ali, Haji Makame Ali, Ibrahim Khamis Fataki, Moza Jaku Hassan, Nassir Ali Juma, Jecha Thabit Komba, Khamis Mbeto Khamis, Mohamed Hassan Moyo, Bhaguanji Mansuria, Moudline C. Castico, Omar Yussuf Mzee, Shamsi Vuai Nahodha, Yakoub Khalfan Shaha, Rose Joel Mihambo, Makame Mnyaa Mbarawa, Ali Omar Mrisho na Mariam Omar Ali.