Na Isri Mohamed

Muigizaji Mkongwe wa Vichekesho Nchini, Yusuph Kaimu maarufu kama Pembe Amefariki dunia Katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Jioni ya Leo Oktoba 20, 2024.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Katibu wa chama Cha Waigizaji Kinondoni, Jafary Makatu.

“Alikuwa anaumwa na alilazwa hospital ya Temeke Kwa siku Tatu”

Muigizaji mwenzake aliyekuwa nae karibu mpaka umauti unamkuta, Mau Fundi, amesema taratibu za mazishi zitatolewa hapo baadae.

Marehemu Pembe alipata umaarufu mkubwa kupitia vichekesho vyake na Senga akiwa na Rungu lake.