Aziza Nangwa,JamhuriMedia, Mtwara
Wananchi na wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wamefurahia elimu ya kupaza sauti juu ya baioanwai ya Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) kuwanufaisha kimaisha kwa kubadili mitanzamo yao Jamhuri imeelezwa.
Mmoja wa wananchi walionufaika na mafunzo ya kupaza sauti za uhifadhi wa baioanwai, Said Stanley, kutoka Kilwa amesema kabla ya mafunzo hayo,walikuwa hawajui umuhimu wa kulinda baioanwai katika kijiji chao walikuwa wakikata miti hovyo na kulima bila ya kujali uhalibifu utakao tokea.
Amesema lakini baada WWF kuwakusanya na kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kushiriki kulinda misitu na faida watakayoipata juu ya utunzaji huo ,walihamasika sana na kuacha mazoea hivyo kupelekea kulinda misitu yao pamoja na wanyama kwa faida yao na taifa.
Stanley amesema mradi huo wa kupaza sauti umefika kwao kwa takribani miaka 10 iliyopita mpaka sasa wananchi wamefundishwa ,namna ya faida ya kuhifadhi, ikolojia ya misitu kwa faida maisha ya baioanwai wote.
Amesema mradi huo umewasadia sana kuweza kufahamu ni namna gani wanaweza kutunza mazingira yao kwa ,faida ya maisha yao kwa kuongeza kipato na kulinda nyara za serikali.
Ameitaja faida ya kwanza wameweza kufikia mafanikio ya kujenga shule ya msingi kwa kutumia pesa wanayoipta kutoka kwenye misitu na wamejiwekea mikakati ya kulipia wanafunzi wanaofauru kwenda sekondar. kiasi cha sh,100,000 kila mwaka.
Amesema faida nyingine ni kwamba wamejenga mazingira ya kumthamini mwanamke kwa kutoa sh.50,000 kwa kila mjamzito anayekaribia kujifungua katika kijiji chao kwa ajili ya kumsadia yeye na mtoto anayezaliwa.
Faida nyingine waliyoipata ni kujenga ofisi yenye thamani ya sh.Milioni 75 kwa kikundi chao amesema asilimia iliyobaki ambayo ni kubwa inakwenda halmashauri na katika ofisi ya kijiji kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wote .
Mpaka sasa kijiji chetu kimeweza kutoa pesa ya kuchimba visima bure na wananchi wanatumia bure bila malipo.
Sihaba Hega kutoka Namtumbo amesema elimu ya uhifadhi katika wilaya yao imewasaidi kuelewa namna ya kuhifadhi mazingira ya misitu yao, na kulinda viumbe hai katika misitu yao ya asili kwa faida ya jamii.
Sihaba amesema uhifadhi umeleta faida kubwa katika vijiji vyao mpaka sasa wamekuwa wanajilipa sh.50.000 kila wanapokusanya wastani wa sh.milioni 100 nyingine ni kwa ajili ya maendelo ya kijiji chao.
Amesema mpaka sasa wameshajenga shule ya msingi nyumba ya mwalimu amesema changamoto iliyopo kwa sasa,baada ya uhifadhi kuwa mkubwa ,ni wanyama kuwa wengi hasa Tembo katika eneo lao wamekuwa wengi na kupelekea ufanya uhalibifu wa kuingia majumbani kuchota nafaka au pombe za kienyeji
kingine ni fidia ndogo kutoka serikalini kulipwa sh.200,000 kama kifuta jasho wakati mazao yaliyoharibiwa ni mengi.
Leticia Mbunda mwenyekiti wa kikundi cha mkoani Ruvuma Masasi amesema elimu ya uhifadhi imewasadia kulejesha wanyama poli kwa wingi na misitu katika eneo lao kwa kiasi kikubwa kuliko huko nyuma.
Amesema wamekuwa na kazi kubwa ya kuelimisha jamii kama wanakikundi wamekuwa mstari wa mbele kwenda sehemu mbalimbali kuelimisha jamii juu ya utunzaji mazingira na viumbe hai kwa manufaa yetu.
Amesema wamekuwa wakienda kwenye shule mbalimbali kuwafundisha wanafunzi juu ya utunzaji wa mazingira ya misitu na wanyama na sasa uhifadhi umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu wananchi wanaelewa faida na wanaiona kwnye maendeleo.