Na Isri Mohamed
Jeshi la polisi Mkoa wa Tabora limethibitisha kifo cha mtoto Ramadhan Sabai (10) kilichotokea kwa kujinyonga juu ya mti wa mwembe.
Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Igunga iliyopo kata ya Malolo, manispaa ya Tabora, ametekeleza tukio hilo akiwa kwa ndugu zake alipokwenda kuwatembelea.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao amesema mtoto huyo amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa na mfuko wa simenti.
Aidha Kamanda Abwao, ameongeza kuwa mara kadhaa akiwa kwa wazazi wake, mtoto huyo amekuwa akijaribu kujinyonga lakini ikashindikana.