Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia
Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa kumnasua mtoto wa kiume wa miaka wa miaka 8 anayesoma shule ya Msingi Mbezi Ubungo Dar es Salaam aliyetekwa Machi 6 , 2025 na Stanley Dismas Ulaya (18) Mkazi wa Kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Kamanda Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi Machi,8, 2025 lilimkamata na baadae kumjeruhi kwa risasi alipojaribu kutoroka chini ya ulinzi walijaribu kumstua kwa risasi za juu lakini alikaidi ikabidi apigwe risasi ya paja na kujeruhiwa hivyo yuko Hospitali Chini ya Jeshi la Polisi akipatiwa matibabu.

“Mtuhumiwa huyo alitekeleza tukio hilo
tarehe 06 Machi, 2025 wakati mtoto huyo aliposhuka katika daladala kabla ya kuingia katika geti la Shule alikamatwa na mtuhumiwa na kumpeleka hadi Bagamoyo Pwani ambako mtuhumiwa alikaa nae vichakani huku akitumia namba ya simu ya mzazi iliyokuwa kwenye madaftari kuipiga huku akidai pesa kwa vitisho ili amuachie na
asimdhuru mtoto huyo na wasipotuma watafuta maiti ” amesema Kamanda
Kamanda Muliro ambainisha kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam lilifanya kazi kubwa ya ziada ya ufuatiliaji na 08 Machi, 2025 majira ya saa 01 :00 usiku baada ya mtuhumiwa kukamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Oysterbay alijaribu kutoroka kwa kukimbia na kulazimika kumpiga risasi mguuni na kwenye paja na kufanikiwa kumzuia baada ya kutotii tahadhari za risasi zilizopigwa hewani awali wakati anakimbia hali yake ni mbaya na
alipelekwa Hospitali kwa matibabu,
Naye Mzazi wa Mtoto huyo Jonson Elisha amesema yeye alimpeleka Mtoto shuleni na kumuacha getini lakini ilipofika jioni Mtoto hakurejea nyumbani ndipo apoanza kumtafuta waalimu wale nao wakamwambia kuna namba inawasumbua awasiliane nayo alipoanza kuwasiliana nayo aliambiwa atume kiasi cha shilingi Milioni 50 ndiyo Mtoto aachiliwe asipotuma atakuta maiti hivyo akaamua kweenda kuripoti kituo cha Polisi ili asaidiwe
Hata hivyo analishukuru Jeshi la Polisi kwa juhudi zao walizozifanya kuwasiliana na kwa mbinu zao na Machi 8, mwaka huu alipigiwa simu aende kituo cha Polisi kuchukua Mtoto na alimkuta akiwa na hali ni njema .
