Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Katavi

Mwanafunzi wa darasa la tatu katika kijiji cha Uruwila Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amejinyonga kwa kutumia sweta lake alipokuwa amelala chumbani kwake.

Akitoa taarifa ya tukio hilo Januari 3, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kasta Ngonyani, amesema tukio hilo limetokea mnamo Januari 2, 2025 Majira ya saa tisa alasiri.

Ameeleza kuwa Matrida Kalibi aligundua kujinyonga kwa mtoto wake Christina Kalilo (8) mwanafunzi wa darasa la tatu.

Ngonyani aliongeza uwa mwanafunzi huyo amejinyonga kwa kutumia sweta lake kwenye chumba alichokuwa amelala.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi imeeleza kuwa chanzo cha kujinyonga kwa mwanafunzi huyo ni kutonunuliwa nguo za Sikuuu ya Khrismas na mwaka mpya.

‘’Chanzo cha kujinyonga ni msongo wa mawazo kutokana na mtoto huyo kutonunuliwa nguo za sikukuu ya Khrismas na Mwaka mpya’’amesema Ngonyani.

Kutokana na tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi amewaomba wazazi na walezi kutimiza majukumu yao kwa kuwatimizia mahitaji yao mhimu ikiwemo mavazi kwakuwa watoto wanahaki ya kupatiwa mahitaji hayo.