Wenyeji, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Nickson Kibabage dakika ya kwanza na Jean Papi Matore dakika ya 29, wakati ya Mbeya City kipa Farouk Shikaro alijifunga dakika ya 55 na Tariq Seif akafunga la pili was dakika ya 65.
Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi nane, ingawa inabaki nafasi ya saba na Mbeya City inafikisha pointi tano katik nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi tano.