Mtalii wa Israel ambaye utambulisho wake haujabainishwa (mwanamke) amefariki na wengine watano kujeruhiwa katika ajali ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili Januari 5, 2025 na Kaimu Meneja Uhusiano wa NCAA, Hamis Dambaya, ajali hiyo iliyotokea Jumamosi usiku wa manane ilihusisha gari la watalii.
“Ajali hiyo ilitokea kati ya eneo la mwonekano na lango kuu la Loduare. Gari hilo lilikuwa na watu saba, sita kati yao wakiwa ni raia wa Israel na Mtanzania mmoja ambaye alikuwa dereva,” ilisema taarifa hiyo.